22/07/2017
UCHAMBUZI WA NOVELA YA NINGALIJUA…
MADOKEZO MUHIMU YA KUZINGATIA
Msanii: Anthony Wambongo
Mwaka wa kuchapisha: 2017
Matbaa: Luminary Adepts Press
Dhamira: Msanii anawausia wasomaji kuhusu athari za kufanya uamuzi bila kuzingatia matokeo yake kwa kina. Anaidhihirishia jamii namna uamuzi wowote ule unavyoweza kuleta furaha au karaha kwa mwamuzi na kwa wategemezi wake.
WAHUSIKA NA UHUSIANO WAO
1. Wahaka - Mhusika mkuu
2. Bashiri - Babaye Wahaka
3. Puaper - Mhusika katika hadithi ya Bashiri
4. Tumaini - Mke wa kwanza wa Wahaka wa mtaa wa Limbukeni
5. Mlowezi - Mnunuzi wa shamba la Pauper
6. Cherezo - Rafikiye wa karibu wa Wahaka (gawadi)
7. Fundo - Mkewe Cherezo
8. Waridi - Mke wa pili wa Wahaka wa mtaa wa Masomaso
9. Kito - Mwanambee wa Wahaka na Tumaini
10. Dafina - Mlungizi wa Wahaka
11. Almasi - Mwana wa tatu
12. Sadiki - Mziwanda (kitindamimba)
13. Dhahabu - Bintiye Wahaka na Waridi
14. Wanuna wa Dhahabu
15. Raufu - Laazizi wa Dhahabu kutoka mtaa wa Masumbuko
16. Msorajua - Babaye Raufu
17. Mashaka - Mamaye Raufu
18. Wanuna wa Raufu
19. Arifu - Rafikiye Raufu kutoka mtaa wa Chengoni
20. Macheche - Mume wa ndoa wa Dhahabu
21. Kachero - Babaye Macheche
22. Saada - Mwanawe Raufu na Dhahabu
23. Shaibu - Tapeli katika mteremko wa Kaskwisha
24. Daraja - Rafikiye Dhahabu waliyesoma naye katika Chuo cha Taamuli
25. Jitu - Mhusika wa ndotoni
26. Memsahib Nadina - Mkewe Kito mwenye asili ya Kizungu
27. Wakili wa Mahak**a ya Jinai ya Tegemeo (MJT)
28. Fr. Oliver O’Brien - Padre Mmishonari mwenye asili ya Kiayalandi
MAUDHUI
1. Tamaa na uchu wa mali
– Pauper anagura shamba lake kwenda kutafuta dhahabu ili ajipatie mali.
- Wahaka anamtelekeza mkewe Tumaini kisha anamwoa Waridi kusudi amzalie mtoto msichana, amwoze ili apate mali k**a wenziwe mtaani.
- Cherezo na Msorajua wanaoza mabinti zao wakiwa bado wadogo kwa ajili ya kujilimbikizia mali.
2. Elimu na mafao yake
- Dhahabu, Raufu, Daraja, Sadiki na kaka zake, wakili wa MJT pamoja na Macheche; wote wanawakilisha tabaka la wasomi watajika wenye elimu kinaifu.
- Elimu huleta mwanga katika jamii.
- Baadhi ya wazazi hususan Tumaini, hutilia uzito suala la wanao kupata elimu ili wawe tofauti katika jamii.
3. Ujinga
- Cherezo na Msorajua wanaendeleza ujinga kwa kukatiza masomo ya wanao kwa kuwaoza mapema.
- Waridi hakuwa msomi, ndio maana hakuweza kuelewa ujumbe uliokuwa katika semansi.
4. Utapeli
- Visa vya kunyang’anya watu baiskeli zao vilikithiri mno hasa kwenye mteremko wa Kasikwisha.
5. Bidii
- Tumaini ni mwenye bidii sana katika kutekeleza majumu yake k**a mzazi.
- Raufu, Dhahabu, na kina Kito wanatia for a masomoni kufuatia juhudi zao za mchwa.
6. Majuto
- Pauper anajutia hatua yake ya kuuza shamba na kuenda kusaka dhahabu kumbe aliiacha dhahabu mle mle shambani mwake.
- Dhahabu na Raufu wanajutia hatua yao ya kuandika waraka wa kujitambulisha kwa Wahaka na Waridi.
- Dhahabu anajutia hatua ya kumwuma Macheche, akidai ndiyo iliyomletea yeye na babaye madhila chungu nzima.
- Tumaini na Kito wanajutia hatua yao ya kumdadisi Wahaka mno kuhusu maisha yake na nyumba ndogo; hali iliyopelekea kuzirai kwa Wahaka.
- Wahaka anajutia hatua yake ya kuwatelekeza wanawe na Tumaini akidhania angekuwa tajiri kutokana na mali aliyotazamia kupata k**a mahari.
- Bila shaka Macheche alijutia kumwoa Dhahabu, kwani alimharibu sura.
- Cherezo alijutia hatua ya kuwachia Wahaka mifugo yake, kwani ilitwaliwa pamoja na ya Wahaka.
7. Imani katika ushirikina (mazingara)
- Wahaka aliamini kuwa Dhahabu na mumewe Macheche walichomekwa mzizi kufuatia mafanikio yao.
- Pia Wahaka alikuwa ameamini kuwa mifugo yake ilikuwa imerogwa.
8. Mapenzi (mahaba) na ndoa
- Kuna ndoa kati ya Wahaka na Tumaini ambayo inatibuka kufuatia tamaa ya Wahaka kutafuta mali.
- Ndoa kati ya Wahaka na Waridi inayojengwa kwa msingi wa uchu wa mtoto na tamaa ya mali.
- Mapenzi ya kweli kati ya Raufu na Dhahabu yanayohitilafiwa na wazazi.
- Ndoa kati ya Macheche na Dhahabu iliyoshabikiwa kufuatia ukwasi wa Macheche.
- Ndoa kati ya Cherezo na Fundo
9. Tanzia
- Bashiri anafariki kutokana na ukongwe.
- Macheche anafariki kufuatia mfadhaiko uliomkumba baada ya kuumwa mdomo na Dhahabu.
- Wahaka anafariki baada ya kukumbwa na kiharusi.
10. Mila na desturi mbovu
- Kukeketa wasichana na kuwaoza mapema (akina Cherezo na Msorajua).
- Kutumia watoto wasichana k**a vitegauchumi na kuwadharau wavulana.
11. Umaskini
- Msorajua na waja wengine wasiokuwa wasomi walikuwa maskini kupindukia.
12. Uraibu wa vileo (ulevi)
- Msorajua ni Daily Drinking Officer (DDO)
- Macheche alikuwa akilewa kila mara.
13. Nafasi ya mwanamke katia jamii
FANI NA MATUMIZI YA LUGHA
1. Sadfa - Coincidence
- Mlowezi anachimba visima vya maji na anaishia kupata vito vyenye dhahabu.
- Dhahabu anarejea nyumbani kutoka mafichoni wakati ambapo huduma za tasnia yake zinahitajika kufuatia mkurupuko wa maradhi ya mifugo (kimeta na ndigana).
- Wahaka anakutana na Cherezo kisadfa viungani mwa mji wa Makutano, kisha Cherezo anamkumbusha kuwa alikuwa amesahau baiskeli yake.
- Dhahabu na Waridi wanaelekea hospitalini kutoka kortini na wanakutana na Daraja, ambaye anawafaa sana katika shida yao.
- Dhahabu na Raufu wanakutana kisadfa wakati Dhahabu anatafuta huduma za wakili.
- Akiwa kwenye kibarua chake katika Jubilee Car Wash, Wahaka anakutana na Tumaini na Kito ambao wamekuja k**a wateja kusafishiwa gari lao.
2. Nahau – Phrasal verbs
- wanaojitia tu hamnazo
- aliwavunja wanawe mbavu
- ota mleli
- shika tariki
- akapigwa na butwaa
- kuasi ukapera
- aliyemjaza pampu
- akayatia kapuni
- alitwikwa zigo la malezi
- akazama akiibuka
- alisimama tisti
- akajifunga nira
- kutia moyo
- kuwa kifua mbele
- onea gere
- alialika nyonda
- fikira za wagivu
- walifumbia macho majukumu ya malezi
- kazi ya kijungujiko
- chuchia kichwa
- achwa kwenye mataa
- chezewa shere
- pandwa na madadi
- chemsha nyongo
- alivunja rekodi
- aliyapa kisogo
- kushika tama
- akasalimu amri
- kitumbua chake kimeingia mchanga
- alirudi nyumbani japo shingo upande
- kufanya tadbiri
- wakifunga pingu za maisha
- akatia mbugi miguuni
- kupiga maji
- kuvaa miwani
- kumpiga mwereka
- akakata kauli
- wacha ale mori
- waliomlilia ngoa
- alienda na ulele nogma
- kupigwa kumbo
- alibiabia
- alichomekwa mzizi
- ikamteka nyara
- mkono wa tahania
- alishikwa na imani
- liligonga mwamba
- huchukua tahadhari
- ameshika tama
- alikaa tutwe
- pumzi zilimpaa
- alichana mbuga
- akili zilipaa
- ilibidi amwite chemba
- alikivunja kimya
- uso wa dhahabu ulidabuka
- kupata ashekali
- kuhesabu pau
- kukata rufaa
- anadaiwa kope si zake
- alipiga moyo konde
- kila mmoja alipata jiko
- aliwakaribisha kwa mikono miwili
- kubwaga moyo
- uso wake uliopiga ndita
- kufua dafu
- aliwachuja wanawe
- kuvuta taswira
3. Methali - Proverbs
- Panapo nia, njia hupatikana.
- Atafutaye hachoki….
- Ndovu halemewi na mkongawe
- Kumtupa jongoo na mti wake
- Asiyekuwa na wake ana Mungu.
- Mungu hamtupi mja wake.
- Dau la mnyonge haliendi joshi.
- Mkono asioweza kuukata, mtu huubusu.
- Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika.
- Chanda chema huvikwa pete.
- Mcheza kwao hutuzwa.
- Mtego bila chambo haunasi.
- Mpanda pantosha huvuna pankwisha
- Ukiona vyaelea, ujue vimeundwa.
- Upweke ni uvundo.
- Cha kuzama hakina rubani.
- Mui hawi mwema (kisanii).
- Pwagu akapata pwaguzi (kisanii).
- Mwenye kovu usidhani kapoa.
- Mchuma janga hula na wa kwao.
- Umdhaniye ndiye, siye.
- Akutukanaye hakuchagulii tusi.
- Usilolijua ni usiku wa giza.
- Likitoka halirudi.
- Mtego wa panya huwanasa waliomo na wasiokuwamo.
- Ng’ombe akivunjikia mguu malishoni, hujikokota hadi zizini.
- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- Mchama ago hanyele, huenda akauya papo.
- Mtu hakatai wito, labda aitiwalo.
- Hata chui ana mkwe
- Mgeni pofu ingawa ana macho yake.
4. Hadithi ndani ya hadithi – Story inside a story
- Hadithi ya Pauper alipoliuza shamba lake na kugura akienda kutafuta dhahabu na kuampulia patupu.
5. Ndoto – Dream (nightmare)
- Jinamizi aliyoota Dhahabu usiku wa kuamkia siku ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake na babaye.
- Ndoto hii ni k**a jazanda inayoonyesha hali ambayo Dhahabu atapitia baadaye.
6. Barua - Letter
- Barua ya kujitambulisha aliyoandika Raufu kwa Wahaka, akampa Arifu kuibaligisha.
- Barua yenyewe inaonyesha namna Raufu alivyokuwa mstaarabu na mwelewa wa utaratibu wa mahusiano.
7. Tashihisi (uhuishi) – Personification
- Macho yake yalijikwaa ghafla kwenye bango – (Pauper)
- Vijumba vilivyosimama kwa wasiwasi mkabala wao – (Masumbuko)
- Alijizatiti kwa udi na ambari kuvumilia madhila haya yote lakini yakakataa katakata kuvumilika – (Dhahabu).
- Kiza kilitishia kumfunika gubigubi – (Wahaka)
- Kibatari kilichowaka kwa wasiwasi mezani – (Numbani kwa Wahaka)
- Kimya kilizidi kushika usukani tangu wakili akipishe – (Kwa Wahaka)
- Gumzo na vicheko vyao vya mara kwa mara vilienda likizo ya ghafla
- Bawaba za mlango zililalamika huku nyumba ikimmeza Wahaka
- Alikuwa amesindikizwa na mavune ajabu.
- Daawa hiyo iliwanyima utulivu.
- Nyuso zenyewe ziliwahukumu – (Kortini)
- Uamuzi huo ulimpokonya Wahaka usemi
- Kimya kilitawala
- Uso wa Dhahabu ulidabuka na kuficha mashaka yake – (Ofisini kwa Raufu)
- Jumba mfano wa kasri lilisimama imara – (Kwa Raufu)
- Hamu ya chakula ilifarakana naye – (Waridi)
- Tangu ulitima umkumbatie – (Wahaka)
- Fikira zake zikajikwaa kwa Dhahabu (Wahaka akiwa Makutano)
8. Taharuki – Suspense
- Pauper auzapo shamba, msomaji anataka kujua ikiwa kweli alipata dhahabu au la.
- Kila mmoja anataka kujua iwapo matamanio ya Wahaka yalitimia.
- Mwandishi anawaacha wasomaji katika hali ya kutaka kujua vile maisha ya Tumaini na wanawe yalivyoendelea.
- Msomaji anataka kujua alikokuwa Dhahabu wakati akiwa mafichoni.
9. Tanakali za sauti – Onomatopoeia
- alitulia nyumbani tuli! – (Dhahabu)
- alishiba vishughuli ndi! – (Macheche)
- kiza kilitishia kumfunika gubigubi – (Wahaka)
- lilitumbukia majini tumwi! na kuzama zii! – (Jitu)
- yameloa jasho chapachapa - (malazi)
- parafujo zilimregea regerege – (Wahaka)
- kumetameta metumetu – (Tumaini)
10. Jazanda – Symbolism
- Kisa cha Pauper.
- Ndoto ya Dhahabu
11. Kinaya – Irony
- Pauper anatarajia kupata dhahabu katika pitapita zake lakini akampulia patupu.
- Wahaka anatajirika kutokana na mahari apewayo lakini anakosa fuaraha.
- Jamii inatarajia kuwa ndoa baina ya Macheche na Dhahabu itadumu lakini inaporomoka baada ya siku chache.
- Jamii inatarajia kuwa Wahaka atasutwa katika mazishi yake, lakini anaishia kusifiwa kupindukia.
- Wahaka na Cherezo wanamwona Tumaini k**a mshinde lakini anaishia kufanikiwa kupindukia.
12. Mahoka – Humour
- Taswira ya kisa cha Wahaka akimgombeza Mashaka kule Masumbuko.
- Vituko vya Macheche akimwekea Dhahabu vikwazo nyumbani kwake.
- Jinsi Wahaka anavyoibiwa baiskeli.
- Jinsi Padre O’Brien anavyoendesha ibada ya mazishi ya Wahaka.
13. Istiara - Metaphor
- tambara mbovu
- pua na mdomo
- mwenye bidii za mchwa
- karamu ya ndovu kumla mwanawe
- alikuwa uyoga mzuri
- mwambie huyo konokono
- alikuwa kiguu na njia
- kuwa mguu niponye
- pumzi za mjusi
- kumbe ukweli ni mchungu
14. Tasfida – Euphemism
- Baada ya kumvumbika Waridi kwa miezi tiza hivi, alipata salama
- Aliwaoza mabinti zake mara tu nguo zao zilipoanza kuinuka vifuani
- ...baada ya kutua mzigo aliotwikwa na Raufu
15. Kejeli – Sacarsm
- Wageni kummiminia marehemu Wahaka sifa asizostahili.
- Kuiombea roho ya marehemu ipumzike kwa amani na kuwasihi watu waige mfano wake.
16. Tashtiti – Satire
- Novela nzima ni tashtiti kwani inakashifu tabia potovu za wazazi; ambazo matokeo yake hudhuru pakubwa jamii zao.
17. Kuchanganya ndimi – Lexicon deviation
- A journey of a thousand miles….. (Raufu)
- Daily Drinking Officer (DDO) – (Msorajua)
- You mean this is all you could ask for? – (Kachero)
- Foolish! Nonsense! Idiot! – (Wahaka)
- Good afternoon Mr. Msorajua – (Daraja)
- Silence! – (Karani wa korti)
18. Majazi –
- Wahaka – wasiwasi
- Tumaini – mtu asiyeangema
- Bashiri – anayetabiri
- Pauper – maskini mwombaji
- Cherezo – mchochezi
- Kito – kitu chenye thamani
- Sadiki – mwenye imani kuu
- Almasi – mwenye thamani kubwa
- Dafina – hazina iliyohifadhiwa chini ardhini
- Dhahabu – mwenye thamani kuu
- Waridi – mrembo (baidhati)
- Saada – tunuku
- Daraja – mvushaji wa watu kutoka dhiki hadi kwenye furaha
- Raufu – mpole (mwungwana)
- Msorajua – asiyekuwa na matumaini
- Mashaka – mwenye dhiki tele
- Chengoni – nyumbani
- Tegemeo – mji wa kutegemewa
- Limbukeni – mahali ambko wakaaji hawana tajriba ifaayo ya maisha
- Masomaso – mahali ambako wakaaji wamechanuka
- Makutano – mahali wanakokutana watu mbalimbali
- Kasikwisha – mteremko unaowamaliza sana watu
- Masumbuko – kijiji chenye dhiki kubwa mno
19. Maswali balagha – Rhetoric questions
- Hayo ni madharau gani? – Wahaka kwa Mashaka
- Mbona ukaamua kumtorosha binti wa wenye navyo ilhali mwenyewe huna hunani? – Mashaka kwa Raufu
- Mume gani huyo ambaye ufukara umechorwa kila mahali usoni pake? – Waridi kwa Raufu
- Na lipi lingekamilika bila ya kuandaliwa karamu ya kukata na shoka? – katika pamvu.
- Lo! Hata chembe ya thamani kwa mkewe hakuiona? – Macheche kwa Dhahabu
- Alitamba huku na kule katika juhudi za kumsaka bintiye ampate wapi? Wahaka akimsaka Dhahabu
- Lakini angejuaje? - Wahaka
20. Tashbihi – Simile
- yalikuwa tu k**a masimulizi ya hekaya za Abunuwas - Wahaka
- walimwenga k**a yai - Dhahabu
- lazima k**a ibada - kukeketwa
- uchungu wa tukio hilo uliokuwa mithili ya shubiri
- k**a mbaazi uliokosa maua
- ndipo Dhahabu alipozuka k**a mzuka jioni moja
- kufafaruka k**a mgonjwa wa kifafa
- kuzubaa k**a saa iliyopoteza majira
- walioachwa nyumbani k**a viokotwe
- wakamwambaa k**a waambaavyo mgonjwa wa ukoma
- walimwandama k**a kupe
- akichakura majalala k**a nzi
- kumetameta metumetu k**a nyota ya alfajiri
- walichopeka macho kwa mwele k**a hadhira inayotazama sinema ya kuogofya
21. Chuku - Exaggeration (hyperbole)
- Vishindo walivyotoa vilitishia kusambaratisha vijumba viwili vya msonge vilivyosimama kwa wasiwasi.
- Tangu watoke katika fungate kule Brussels, Ubelgiji, Dhahabu hakujua jingine ila upweke uliomzingira.
- Namna wazungumzaji wanavyommiminia marehemu Wahaka sifa tele.
22. Takriri – Idiom
- miaka na mikaka
- kataa katakata
- hayamhusu ndewe wala sikio
- waliishi raha mustarehe
- aliyesubiri kwa hamu na hamumu
- kufumba na kufumbua
- alieleza kinaganaga
- kwa hali na mali
- wakaandamana guu mosi guu pili
- Wahaka na Waridi walibaki mahawinde bila mbele wala nyuma
- kukaa bila kazi wala bazi
23. Kisengere nyuma – Flashback
- Awali katika majira ya alasiri, mgeni ajinabi aliwasili nyumbani na kumpata Dhahabu akiwa pekee yake
- Alikumbuka cheche za matusi alizowatolea wazazi wa Raufu kule masumbuko
24. Kisengere mbele – Foresight
- Ilibidi ajiunge na chuo hicho mwaka uliofuata
- Mahak**a ilimwakiza Dhahabu na babake kufika mbele ya hakimu siku mbili baadaye ili kufunguliwa mashtaka.
- Maiti alipelekwa kenyekenye hadi ufuoni, huku wao wakiasisi mipango ya mazishi ambayo yangefanyika kijijini Limbukeni wikendi hiyo hiyo.
SIFA (SILIKA) ZA WAHUSIKA – CHARACTER TRAITS
• Tumia vivumishi sifa kusawiri tabia za wahusika. Km:
Wahaka: - Limbukeni, mwenye mapuuza, msahaulifu, mwenye tamaa.
Tumaini – Mwenye bidii, mvumilivu, msalihina.
Macheche: Mgobo (mchokozi), mtaaradhi, mwenye kisasi.
Dhahabu: - Mkak**avu, mvumilivu, msiri, mjuzi wa kazi yake.
Kachero: - Mwenye majikwezo, karimu.
FUNZO MAALUM KATIA KAZI YA NINGALIJUA…
• Wazazi wasiwatumie watoto k**a vitegauchumi.
• Tufanye bidii tukimtegemea Mwenyezi Mungu
• Tuepukane na marafiki wapotovu k**a Cherezo.
• Tuwasamehe waliotukose lakini tusiyarudie makosa yao.
• Hakuna kinachowezekana kabla ya wakati wake
• Mungu hamtupi mja wake.
• Liandikwalo halifutiki.
• Fimbo ya mbali haiui nyoka